Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limewaua “dazeni” za wapiganaji wa Hamas usiku kucha, huku likiimarisha operesheni zake za ardhini huko Gaza.
Ilisema katika taarifa: “Wakati wa mapigano na magaidi katika Ukanda wa Gaza, askari wa IDF waliwaua makumi ya magaidi ambao walijifunga kwenye majengo na vichuguu, na kujaribu kuwashambulia wanajeshi.
“Katika tukio moja, ndege ya IDF iliyoongozwa na askari wa ardhini wa IDF iligonga nguzo ndani ya jengo la shirika la kigaidi la Hamas, ikiwa na zaidi ya wapiganaji 20 wa Hamas ndani yake.
“Kwa kuongeza, katika siku chache zilizopita, IDF ilipiga shabaha zaidi ya 600, ikiwa ni pamoja na maghala ya silaha, maeneo kadhaa ya kurusha makombora ya vifaru, pamoja na maficho na viwanja vinavyotumiwa na kundi la kigaidi la Hamas.
“Usiku mmoja, wanajeshi wa IDF walitambua magaidi wenye silaha na kituo cha kurusha kombora la kifaru katika eneo la Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na kuiongoza ndege ya kivita kuwashambulia.”