Kwa kawaida mtu anapoaga dunia, atawaachia wanafamilia zao mali yoyote waliyokusanya lakini hii haikuwa hivyo kwa Ben Rea (Uingereza) na paka wake kipenzi Blackie.
Blackie alisalia pauni milioni 7 (dola milioni 12.5) sawa na zaidi ya billioni 21 wakati mfanyabiashara huyo mamilionea wa vitu vya kale alipokufa mnamo 1988.
Urithi mkubwa ulimfanya Blackie kuwa paka tajiri zaidi duniani, rekodi ambayo bado iko leo.
Mmiliki wa paka Blackie Ben alipata bahati yake ya kununua na kuuza vitu vya kale, ambayo ilimruhusu kuwapa paka wake maisha ya kupendeza ambayo alihisi wanastahili.
Na Blackie alikuwa paka wake, wa mwisho kuishi kati ya paka 15 walioishi na Ben katika jumba lake la kifahari huko Dorney, Buckinghamshire, ambaye alirithi pesa hizo.
Ben alikuwa na familia, lakini alijitenga na alikataa kutambua familia yake katika mahusiano yake ndani ya maisha yake
Na baada ya kifo chake , pesa zake nyingi ziligawanywa kati ya mashirika matatu ya kutoa msaada ya paka pamoja na maagizo kwamba walipaswa kumchunga kipenzi chake huyo hadi siku yake ya mwisho.
Ben pia alitoa kiasi kidogo cha mamilioni yake kwa mtunza bustani na fundi wake.
Hii ni tofauti na rekodi tajiri zaidi ya mbwa, ambayo ilipunguzwa wakati hadithi yake ivyoanza kuleta utata
Gunther the German Shepherd aliripotiwa kukabidhiwa dola milioni 65 (pauni milioni 40) wakati mmiliki wake Countess Karlotta Liebenstein alipofariki.
Ulimwengu mzima ulivutiwa na hadithi ya Gunther,na hii ni kulingana na Guinness world record walipojumuisha rekodi hiyo katika kitabu cha rekodi mwaka 1998.
Kulingana na Guinness paka Blackie na mbwa Gunther sio wanyama pekee walioingia kwenye rekodi huko nje.
Inadaiwa kuwa paka mwingine maarufu kwenye mtandao wana thamani ya mamilioni, kama vile paka wa Taylor Swift Olivia Benson na Grumpy Cat, ingawa bila shaka, wao wenyewe hawana pesa hizo ila wamemilikishwa tu.
Lakini kiufundi, pesa za Ben zilihusishwa na Blackie milele, na mashirika ya misaada hayakuweza kupokea pesa isipokuwa walikubali kumtunza paka.yaani no matunzo no money. Tujiulize hata ingelikuwa ni wewe kwa pesa hizi ungekataa kumtunza?
Na Ben hakuwa mtu pekee aliyewahi kutoa mamilioni yake kwa wanyama wake wa kipenzi.
Siku chache kabla ya kifo cha huzuni cha Ben, dada yake pia alikufa na kuacha £ 2 milioni kwenye shirika la misaada ya wanyama.
Mbunifu mashuhuri wa mitindo wa Chanel Karl Lagerfeld anasemekana kuwa alimwachia paka wake wa rangi ya bluu Birman Choupette dola milioni 1.5 alipofariki mwaka wa 2019.
Choupette alipata umaarufu kutokana na mmiliki wake, huku watu mashuhuri akiwemo mwigizaji Jared Leto hata akivalia kama yeye kwenye event ya Met Gala ya 2023, ambayo ilikuwa na mada ya kuikumbuka heshima ya mbunifu marehemu.
Haijulikani mengi kuhusu kilichomtokea Blackie baada ya kifo cha Ben, na kama bado yu hai leo na anaendelea kufurahia maisha yake ya milionea.