Mwanzilishi Jukwaa la ujumbe la Telegram litazuia chaneli zilizoitisha vurugu dhidi ya Wayahudi katika eneo la Dagestan nchini Urusi alisema mwanzilishi wa jukwaa hilo Pavel Durov.
“Chaneli zinazoitisha vurugu zitafungwa kwa kukiuka sheria za Telegram, Google, Apple na ulimwengu mzima uliostaarabika,” Durov aliandika kwenye chaneli yake ya Telegram.
Pia alichapisha picha ya skrini kutoka “Utro Dagestan” (Morning Dagestan), chaneli ambayo ilikuwa na vitisho kwa jamii ndogo ya Wayahudi wanaoishi Dagestan.
Urusi imewakamata takriban watu 60 kuhusiana na ghasia hizo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.
Shirika la Usafiri wa Anga la Shirikisho la nchi hiyo lilizuia kwa muda safari zote za ndege kwenda na kutoka uwanja wa ndege baada ya ghasia, kisha ikatangaza Jumatatu asubuhi kwamba safari nyingi za ndege zitaanza tena, isipokuwa kwa ndege za Tel Aviv, ambazo zimesimamishwa kwa muda usiojulikana.