Klabu ya Real Madrid inaripotiwa kuwa inalenga kuwanunua Erling Haaland na Kylian Mbappe katika miaka ijayo. Kulingana na gazeti la Uhispania El Chiringuito kupitia jarida la 90 minutes wakuu wa Real Madrid hawakati tamaa ya kuwarubuni Mbappe na Haaland Bernabeu, ingawa si kwa wakati mmoja.
Nia ya Real kumnunua mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Mbappe imethibitishwa kwa miaka mingi, huku miamba hao wa La Liga wakijaribu kumtorosha kutoka mji mkuu wa Ufaransa kwa dau la dakika za mwisho la pauni milioni 171.7 siku ya mwisho ya dirisha la kiangazi 2021.
Dalili zote zilionyesha Mbappe kujiunga na Real kwa uhamisho wa bure mnamo 2022, lakini alipuuza Los Blancos kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na PSG, ambao unamalizika mwishoni mwa kampeni ya sasa.
TAZAMA PIA…