Hospitali kubwa zaidi ya Gaza iko kwenye hali mbaya kutokana na jenereta zake kutofanya kazi, daktari ameiambia vyombo vya habari.
Dk Omar Abdel-Mannan alisema amekuwa akiwasiliana na wataalamu wa matibabu katika Hospitali ya al Shifa “kila siku” na hali ni mbaya
“Wasiwasi mkubwa niliokuwa nao jana usiku ni ujumbe wa mwisho niliopokea kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ni kwamba walikuwa saa kadhaa mbali na jenereta katika hospitali ya al Shifa… hazifanyi kazi tena,” alisema.
Akifafanua maana yake, alisema taa zitazimika, viingilizi vitaacha kufanya kazi, watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wao “watakuwa wanakufa” na “wale wanaotumia dialysis kila siku watakufa”.
“Kwa kweli hili ni janga la kibinadamu zaidi ya chochote ambacho tumeshuhudia katika historia ya hivi karibuni,” daktari wa watoto aliongeza.
Alisema ameona picha za watoto wakiwa na “viungo vilivyovunjwa viungo, miili iliyoharibika, walioungua usoni” na “hakuna dawa za kuwapa”.
“Ni afadhali wafe, huo ndio ukweli,” alisema.
“Wako katika maumivu na uchungu kabisa.”