Benjamin Netanyahu ameonya kuhusu vita “vikali” na “muda mrefu” mbele, baada ya wanajeshi kadhaa wa IDF kuuawa wakati wa mapigano kaskazini mwa Gaza.
Katika video iliyotumwa kwa X, waziri mkuu wa Israel alizungumzia “hasara chungu”.
“Taifa zima la Israeli linawakumbatia ninyi, familia, kutoka ndani ya mioyo yetu,” alisema, akiongeza kuwa Israeli itaendeleza misheni yake “hadi ushindi”.
Idadi ya Wapalestina waliouawa huko Gaza hadi sasa imeongezeka hadi 8,796, wizara ya afya inayoongozwa na Hamas imesema.
Miongoni mwa waliofariki ni watoto 3,648, ilisema.
Idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 8,525 vilivyoripotiwa na wizara hapo jana