Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto, ambayo imeshutumu “ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto” katika Ukanda wa Gaza. Kamati hiyo “inalaani vikali kuongezeka kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya malengo ya kiraia katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha vifo vya watoto zaidi ya 3,500 tangu Oktoba 7, 2023” na pia inasema “ina wasiwasi mkubwa” juu ya hatima ya watoto wanaoendelea kushikiliwa na Hamas.
Utawala wa kifalme wa Ghuba umechukua jukumu la mpatanishi katika uhamishaji wa wageni na waliojeruhiwa kwenda Misri, na pia umeingilia kati mazungumzo ya kuwaweka huru mateka walioshikiliwa huko Gaza. Hatimaye, nchi hiyo inawapa hifadhi maafisa wakuu wa Hamas walio uhamishoni, kama vile nambari moja wa vuguvugu hilo, Ismaël Haniyeh.
Majeruhi 76, wageni 335 na raia wenye uraia pacha wamehamishwa kutoka Gaza hadi Misri, kulingana na afisa wa Misri. Kulingana na Quai d’Orsay, watu watano, raia wa Ufaransa ni miongoni mwa waliohamishwa.
Wanajeshi 15 wa Israel wameuawa katika muda wa saa 24 huko Gaza