UNICEF Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, kila siku zaidi ya watoto 400 wanauawa au kujeruhiwa huko Gaza kutokana na uvamizi wa Israel.
Katika taarifa yake, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa takriban watoto 3,500 wameripotiwa kuuawa, huku zaidi ya 6,800 wakijeruhiwa kutokana na “mashambulizi ya mabomu” yanayoendelea.
“Hii haiwezi kuwa hali mpya ya kawaida,” ilisisitiza, na kuongeza, “Watoto wamevumilia kupita kiasi tayari. Mauaji na utumwa wa watoto lazima ukomeshwe. Watoto si walengwa.”
Huku hayo yakiri[potiwa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linakadiria kuwa licha ya kuhamishwa awali kwa wamiliki wa pasipoti za kigeni na Wapalestina kujeruhiwa vibaya katika mpaka wa Misri, zaidi ya watu 20,000 waliojeruhiwa bado wamekwama katika Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano MSF ilisema kuwa katika uhamishwaji huo “idadi ya watu waliojeruhiwa vibaya”, miongoni mwao wafanyakazi wake 22 wa kimataifa waliondoka Gaza kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah.