Utawala wa rais wa Marekani Biden ulisema utaandaa mkakati wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu huku kukiwa na mvutano wa nchi nzima tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas.
“Rais Biden aligombea madaraka ili kurejesha roho ya taifa letu. Hana shaka: hakuna mahali pa chuki Marekani dhidi ya mtu yeyote. Kipindi,” msemaji wa Ikulu ya White House Karine Jean-Pierre.
“Kwa muda mrefu sana, Waislamu nchini Marekani, na wale wanaochukuliwa kuwa Waislamu, kama vile Waarabu na Masingasinga, wamevumilia idadi kubwa ya mashambulizi yanayochochewa na chuki na matukio mengine ya kibaguzi,” aliongeza.
Mkakati huo utaandaliwa kufuatia majadiliano na jamii husika. White House pia ilitaja mauaji ya hivi karibuni “ya kinyama” ya mvulana Mpalestina Mmarekani mwenye umri wa miaka sita nje ya Chicago ambayo polisi wamehusisha na vita vinavyoendelea.
Haya yanajiri huku serikali ya Marekani ikiwa tayari imezindua mpango wa kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi kote nchini.