Mwanamume mmoja amekamatwa kwa tuhuma za uharibifu na uhalifu baada ya maandamano huko Piccadilly katikati mwa London.
Kukamatwa huko kumekuja baada ya jumbe kuhusu mzozo wa Israel na Hamas kuandikwa kwa rangi nyekundu kwenye jengo, Polisi wa Met walisema kwenye X, wakishiriki picha inayoonyesha uharibifu huo.
Mtu wa pili alionekana yuko kwenye dari juu ya mlango wa jengo hilo.
“Maafisa wanashughulika na mtu huyu na pindi atakapokuwa chini salama watatafuta kumkamata kwa makosa yoyote,” Met alisema.
Wanaharakati pia walilenga Ofisi ya Mambo ya Nje, wakipaka rangi nyekundu kwenye mlango wa jengo na kuandika ‘blood’.