Mwenyekiti wa Baraza la Utawala nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan ametoa amri ya kuwafuta kazi mawaziri watano wa wizara za nishati na mafuta, biashara na usambazaji, uchukuzi, kazi na mageuzi ya kiutawala, na mifugo.
Pia ameipanga upya wizara ya nishati na mafuta kuwa wizara ya nishati na madini na kuwateua mawaziri wanne wapya wa kushughulikia mambo ya nishati na madini, biashara na usambazaji, uchukuzi, na kazi na mageuzi ya kiutawala.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyu kubadilisha maofisa wa ngazi ya uwaziri tangu mgogoro ulipuke mwezi Aprili mwaka huu nchini humo.