Mkurugenzi wa Ofisi ya kamishna mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa mjini New York amejiuzulu akilalamikia jinai zunazoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza.
Craig Mokhiber, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa huko New York, ameandika katika barua yake ya kujiuzulu kwamba, “kwa uchungu mkubwa imebainika kwamba, Umoja wa Mataifa unazembea kutekeleza wajibu wake wa kuzuia ukatili, kuwalinda wanyonge na kuwawajibisha wahusika.”
Kwa mujibu wa afisa huyu wa juu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, “mauaji ya kimbari yanafanyika sasa mbele ya macho ya walimwengu”.
Haya yanajiri sambamba na mashambulizi makali na ya kikatili yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina. Eneo hili linaendelea kushambuliwa kwa silaha nzito na za kisasa za utawala wa Kizayuni wa Israel kutokea nchi kavu, baharini na angani.