Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio la kumpongeza Spika wa Bunge la Tanzania, Dk.Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Akiwasilisha hoja ya kuliomba bunge lipitishe azimio la kumpongeza Dk.Tulia, Mbunge kutoka Tanzania Dk.Shogo Sedoyeka, katika mkutano wa bunge hilo ulioanza jijini Arusha, alisema uwakilishi wa Dk.Tulia siyo kwa ajili ya Tanzania pekee, bali ni alama ya uwezo wa uongozi kwa wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Afrika kwa ujumla.
“Wanawake wanaweza na huu ushindi wa Dk.Tulia ni jibu tosha kwa nchi za Afrika na EAC, kuwa wanawake wanaweza kuongoza nafasi mbalimbali ngazi za juu, ikiwemo vijana kutumia fursa za kugombea nafasi mbalimbali bila kuogopa na kuondoa hofu,”alisema.