Eneo la Mpeketoni Kenya limekumbwa na shambulizi jingine ambalo limetokea karibu na Lamu , Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi hilo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu 50 mpaka sasa.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab limekiri kufanya mashambulizi hayo na kusema kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
Takribani watu 50 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.