Katika kipindi cha siku za hivi karibuni kundi la kigaidi la Boko haram limeua watu 40 nchini Nigeria.
Shughuli za magenge yenye silaha zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni nchini Nigeria, ambapo makundi hayo yamevuruga usalama kwa kuteka nyara, kupora na kuharibu mali za watu na kuua raia wa eneo hilo.
Maafisa wa polisi ya Nigeria walitangaza Jumatano kwamba katika siku za hivi karibuni raia wasiopungua 40 wameuawa katika shambulio la magaidi wa Boko Haram kwenye jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti za eneo hilo, magaidi wa Boko Haram wameua watu 17 kwa kuwafyatulia risasi wanakijiji katika jimbo la Yobe.
Siku ya Jumanne magaidi hao pia walitega mgodi na kuulipua na kuua wanakijiji wasiopungua 20 waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka sehemu ya kuzika maiti siku iliyotangulia.
Boko Haram pia wameteka nyara na kuua watu kadhaa katika jimbo la Borno.
Jimbo hilo limekuwa kitovu cha uasi na machafuko nchini Nigeria kwa miaka 14.Kwa kuenea vitendo vya kigaidi, hatimaye Rais Bola Tinuba wa Nigeria na baraza lake la mawaziri walipitisha bajeti ya dola bilioni 2.8 kwa ajili ya kuimarisha sekta ya kijeshi na usalama ya nchi hiyo.