Zaidi ya raia 20 waliuawa Jumapili jioni, Novemba 5, wakati makombora yalipoanguka kwenye soko huko Omdurman, kitongoji kilicho karibu na Khartoum, mji mkuu wa Sudan, shirika moja lisilo la kiserikali limetangaza.
Kulingana na taarifa kutoka kwa Kamati ya Wanasheria wanaounga mkono Demokrasia ambayo inaandika kumbukumbu za vifo vya kiraia na ukiukwaji wa haki za binadamu katika mzozo huo, “wakati wa majibizano makali ya risasi kati ya wapiganaji, makombora yalianguka kwenye soko la Omdurman.” “Zaidi ya raia 20 waliuawa na wengine kujeruhiwa,” inasema taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.
Siku moja kabla, angalau raia 15 waliuawa na “baada ya kuangukiwa na makombora kwenye nyumba zao” huko Khartoum, chanzo cha hospitali kimesema.
Vita kati ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo Aprili 15 vilivyoanza Aprili 15, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (Acled), huku wadadisi wakisema idadi hiyo inaweza kuwa juu zaidi.