Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema Jumatatu ilikuwa ikiwaondoa kwa muda baadhi ya wafanyikazi wa ubalozi wa Uingereza kutoka Lebanon.
Ilikuwa tayari imewashauri Waingereza dhidi ya safari zote za kwenda Lebanon kutokana na mzozo kati ya Israel na Gaza, na kuwahimiza Waingereza wowote ambao bado wako nchini kuondoka wakati safari za ndege za kibiashara zikisalia.
Mwongozo wa sasa wa Ofisi ya Mambo ya Nje pia unashauri dhidi ya safari zote za kwenda Lebanon huku kukiwa na mvutano mkali kwenye mpaka na Israeli.
Wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Hezbollah na washirika wao wamekuwa wakipambana kwa muda wa mwezi mmoja mpakani tangu kuanza kwa vita vya Israel na Hamas.