Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria Jay Jay Okocha amemlaumu kocha wa timu hiyo kwa matokeo mabaya iliyopata timu ya Nigeria kwenye mechi ya kombe la dunia vs Iran June 16 ambapo timu hizo zilicheza mechi ya kwanza ya sare ya bila kufungana katika michuano hiyo.
Okocha amesema >>’Mechi hii ilipaswa kuwa ya ushindi wa Nigeria lakini hatukujitosa kimasomaso kushinda, hatukufanya vyema na tulishindwa kabisa, kocha Keshi hakufanya kazi ya kutosha kuandaa timu na ndio maana game haikua nzuri hata kidogo… Kocha anapaswa kuwajibika’.
Wataalamu wa soka wamedai kuwa mechi kati ya Nigeria na Iran haikuwa ya kusisimua kama mechi nyingine ambazo zimechezwa mpaka sasa ambapo hii stori imeongezewa uzito baada ya hiyo kauli ya Okocha ambae kwa sasa yuko kwenye kamati ya timu ya taifa ya Nigeria.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB