Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney ameelezea matumizi yake ya unywaji pombe mapema katika maisha yake ya soka kuwa “afadhali yamepita”.
Meneja wa Birmingham alionekana kwenye podikasti mpya ya nyota wa zamani wa ligi ya raga na mwanaharakati wa Ugonjwa wa Motor Neurone Rob Burrow, na kufunguka kuhusu matatizo aliyokumbana nayo katika kutafuta njia ya kukabiliana na shinikizo la umaarufu alipokuwa kijana.
Rooney aliingia kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Everton akiwa na umri wa miaka 16, akawa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 17, na alijiunga na Manchester United akiwa na umri wa miaka 20, lakini amesema kiwango chake cha juu kilitokana na gharama.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alimwambia Burrow: “ahuweni kwangu ilikuwa kwenye pombe nilipokuwa na umri wa miaka 20 kwani ningeenda nyumbani, na kukaa siku kadhaa nyumbani na kutotoka ningekunywa karibu kufa
“Sikutaka kuwa karibu na watu, kwa sababu wakati mwingine naona aibu. Wakati mwingine unahisi kuwa umewaangusha watu na mwishowe sikujua jinsi ya kukabiliana nayo.
“Usipochukua msaada na mwongozo wa wengine, unaweza kuwa katika hali ya chini sana, na nilikuwa na hilo kwa miaka michache. Nashukuru, sasa siogopi kwenda kuzungumza na watu kuhusu masuala haya kwani nimeacha. “