Kesi 940 za ukiukwaji wa haki za binadamu na dhulma mbalimbali zimerekodiwa nchini DRC kwa miezi ya Julai na Agosti 2023 pekee, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde kutoka ofisi za pamoja za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa (UNJHRO). Idadi inayoongezeka ikilinganishwa na miezi iliyopita, pia kunaripotiwa ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kijinsia.
Hili ndilo jambo lililoangaziwa katika ripoti hii, ongezeko hili la waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia: Kesi 120 zilirekodiwa na UNJHRO, 49 mwezi Julai, 71 mwezi Agosti, nyingi zikiwa ni za wapiganaji wa makundi yenye silaha.
Unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na migogoro iliyotambuliwa kupitia tume kadhaa za uchunguzi kuhusiana na tatizo hili, unaeleza Umoja wa Mataifa, katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa, kwa mfano katika majimbo ya Maniema na Tanganyika.
Na kile ambacho ni halali kwa unyanyasaji wa kijinsia pia ni halali kwa ukiukaji wa haki za binadamu na dhulma, ambao wengi wao wanawajibika kwa makundi yenye silaha.
Lakini ripoti hiyo bado inabainisha kuwa mwezi Agosti, kulikuwa na ongezeko la idadi ya ukiukaji unaohusishwa na maafisa wa serikali katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Haut-Katanga na Kinshasa. Wakati huu inahusu hasa kukamatwa na kufungwa kiholela.