Familia ya muigizaji maarufu wa vichekesho wa Nigeria John Okafor, anayejulikana zaidi kama Bw Ibu, inasema mguu wake umekatwa kwa sababu za kiafya.
Madaktari hawakuwa na budi ila kumkata kiungo huyo “ili kumuweka hai”, jamaa zake walisema katika taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Hali hii imekuwa magumu kwetu sote lakini tumelazimika kuikubali kama hali mpya ya Baba,” wameandika.
Okafor, mwenye umri wa miaka 62, ameigiza katika filamu nyingi za Nollywood zikiwemo Keziah, 9 Wives na Mr Ibu jijini London.
Familia yake haijafichua chanzo cha ugonjwa huo uliosababisha kukatwa kwa mguu wake.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa mwigizaji huyo amefanyiwa upasuaji mara saba na anahitaji kufanyiwa upasuaji mwingine mmoja zaidi.
Vyombo vya habari vya Nigeria vinaripoti kuwa baadhi ya gharama za matibabu za Okafor zimelipwa na aliyekuwa Rais wa Seneti Bukola Saraki.
Familia yake inawaomba mashabiki na watu wema walipe salio, bila kutaja kiasi hicho.
Rufaa kama hizo kutoka kwa waigizaji wa Nollywood si jambo la kawaida, anasema mwandishi wa BBC Annette Arotiba nchini Nigeria.