Mapigano yanaendelea katika Ukanda wa Gaza, sasa yamegawanya eneo hilo hehemu mbili. Mashambulio ya mabomu yanaatahiri raia, ikiwa ni pamoja na kusini mwa eneo hilo. Mapema wiki hii Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake itakuwa na “jukumu la jumla la usalama” wa Ukanda wa Gaza kwa muda usiojulikana mara baada ya vita na Hamas kumalizika.
Siku ya Jumanne Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant alihakikisha kwamba jeshi la Israeli liko “katikati ya Jiji la Gaza” na kwamba wanajeshi wake “wataangamiza Hamas”. Aliita Gaza “kambi kubwa zaidi ya magaidi kuwahi kujengwa.”
Benyamin Netanyahu amebaini kwamba hakutakuwa na usitishaji vita au mafuta kuruhusiwa kuingia huko Gaza hadi Hamas iwaachilie mateka 240 inayowashikilia. Waziri Mkuu pia ameonya Hezbollah ya Lebanon kwamba itafanya “kosa la maisha yake” ikiwa itajiunga na mzozo ulioanzishwa na Hamas. Israeli inakubali tu kuzingatia uwezekano wa “kusitisha mashambulizi yake kwa muda mfupi” .
Washington inaonya kwamba haitaunga mkono kukaliwa kwa Gaza na Israel, baada ya Netanyahu kutangaza kwamba anataka kuchukua “jukumu la jumla kwa ajili ya usalama” wa eneo hilo baada ya vita.