Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima ameonesha kukerwa na watu wanaofanya uharibifu kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kufanya shughuli za kibinadamu kama Kilimo,ukataji mkaa na uchimbaji madini.
Rc Malima ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa maji wa Kiburubutu Ifakara ambapo amesema licha ya serikali kutoa fedha nyingi miradi ya maji lakini baadhi ya watu wakikwamisha miradi hiyo na kusababisha kufanya kazi muda mchache na kushindwa kuendelea.
Amesema jambo hilo halikubaliki kwani wananchi wanahitaji huduma hivyo serikali haitakubali na kuwafumbia macho wananchi wasipate huduma ya maji huku fedha za serikali zikipotea bure bila sababu ya msingi
Amesema mpango wa serikali ni kuwahudumia wananchi wa mjini na vijijini wote wapate sawa huduma za kijamii hivyo uharibifu huo umekua kikwazo kwenye miradi mingi ya maji na kushindwa kutoa huduma kwa wa sababu ya maslahi ya watu wachache yeyote atakaye kamatwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
“nimekuja hapa kwenye chanzo ili nione huu mradi kama utakua na uhai mana tunaweza kujenga mradi wa ,mabilioni ya fedha alafu ikashindwa kutoa huduma kisa uharibifu mazingira na vyanzo vya maji”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira Ifakara (IFAUWASA)Mhandisi Ahmad Mpambaike amesema Mradi wa maji Kiburubutu unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2025 na utagharimu fedha kiasi cha shilingi Bilioni 42
Mhandisi Mpambaike amesema hali ya sasa utoaji Huduma ya maji Mji wa Ifakara ni asilimia 34 ambapo mradi huo umefikia asilimia 7 ya utekelezaji wa ujenzi wake na unasimamiwa na mkandarasi mashauri (Consultant) WAPCOS LIMITED INDIA na Mkandarasi Mjenzi (Contractor) Larsen &Toubro Limited India.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamemshukiru Rais Samia Suluhu Hasaan kwa mradi huo na kwamba endapo utakamilika utasaidia kupatikana huduma ya maji pamoja na kuchochea maendeleo kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.