Habari kutoka polisi wa Nepal inasema tetemeko la ardhi lililotokea usiku wa manane wa tarehe 3 magharibi mwa nchi hiyo limesababisha vifo vya watu 157 na wengine karibu 170 kujeruhiwa.
Kwa sasa serikali ya Nepal imeweka kipaumbele kwenye kazi ya uokoaji ambapo askari polisi na jeshi wanashiriki katika kazi hiyo. Chama cha Congress cha Nepal na Chama cha Rastriya Swatantra vimetoa fedha za msaada wenye thamani ya takriban dola za Kimarekani 37,600 kwa maeneo yaliyoathirika na kupanga vikundi viwili vya madaktari kushiriki katika uokoaji.
Msaidizi wa mkuu wa wilaya za Jajarkot, moja kati ya wilaya mbili zilizokumbwa na tetemeko hilo, ameliambia shirika la habari la Xinhua kuwa kuna majeruhi wengi katika wilaya hiyo, na miundombinu na rasilimali watu havitoshi kukabiliana na hali hii ya dharura