Baada ya kilio cha Mda mrefu kuwepo katika Klabu ya Geita Queens inayoshirikia ligi kuu ya wanawake kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukata wa kifedha Hatimaye Kilio chao kimesikika kwa Wadau wa Maendeleo ambapo Wamepata Vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari wakati wa Makabidhiano ya Vifaa hivyo Vikiwemo Jezi pamoja n Taulo za Kike Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Bi.Zahara Michuzi amesema Vifaa hivyo vitaenda kuwa chachu ya kuisukuma klabu kufanya vizuri katika Ligi huku akiwataka wadau kuendelea kujitokeza zaidi kutoa Misaada.
“Mradi huu kwetu umekuwa ni chachu ya kupunguza vitendo vya kikatili majumbani Mashuleni mitaani kwa kushirikiana na hawa wenzetu kuonyesha tija kwenye hili na huu msaada wanaotuletea hapa msaada ambao utawagusa wengi zaidi watoto wote tulio nao kwenye Geita Queens wanatoka katika Familia duni , ” Mkurugenzi Michuzi.
Kwa upande wake Meneja Mradi KAGS kutoka shirika la Rafiki SDO , Eliud Mtayuga amesema lengo la Vifaa hivyo kuisaidia klabu hiyo ambayo hapo mwanzo ilikuwa na ukata wa vifaa vya michezo ambapo zoezi hilo limekamilishwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita huku vikigharimu kiasia cha Shilingi milioni 4.
Mtayuga amesema kama shirika wataendelea kushirikiana na Klabu hiyo ambapo amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Geita Bi, Zahara Michuzi kwa kukubari na kuwa sehemu ya uhitaji kwa klabu ya wanawake Geita Queens yenye Maskani yake Mkoani Geita.
Salumu Kurunge ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu GEREFA mkoa wa Geita amesisitiza watanzania pamoja na wananchi wa Geita kuendelea kuiunga Mkono klabu ya Geita Queens inayoshiriki Michuano ya Ligi kuu ya Wanawake hapa nchini huku akilishukuru Shirika la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na Mradi wa Plani International kupitia Mradi wa KAGS.