Duru moja iliyo karibu na Hamas imeripoti kuwa Qatar inafanya upatanishi kwa ajili ya kutekelezwa usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, duru moja iliyo karibu na harakati ya Hamas imetangaza leo kuwa mazungumzo yanaendelea na utawala wa Kizayuni kwa upatanishi wa Qatar kuhusiana na kutekelezwa usitishaji vita wa siku tatu kwa ajili ya kuwaachia huru mateka 12, ambao nusu yao ni Wamarekani.
Kabla ya hapo, Abu Ubaidah, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS, alisema idadi ya mateka wa Kizayuni wanaoshikiliwa huko Gaza inakaribia watu 250, ambapo 200 wako mikononi mwa tawi la kijeshi la harakati hiyo la Brigedi za Izzuddin al-Qassam na waliosalia wanashikiliwa na makundi mengine ya muqawama.
Katika maandamano yaliyoishia kwenye mkusanyiko huo, familia za mateka wa Israel zilimtaka waziri mkuu wa utawala huo ghasibu Benjamin Netanyahu, asimamishe vita haraka iwezekanavyo na kuchukua hatua kwa ajili ya ubadilishanaji wa mateka.