Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone alitia saini mkataba wa nyongeza Alhamisi ili kusalia katika klabu hiyo hadi Juni 2027.
Atletico ilisema kuongeza mkataba wake na kocha huyo wa Argentina kunatoa “mwendelezo” wa mradi huo ambao ulianza alipowasili Desemba 2011.
“Tangu wakati huo, taasisi yetu imepitia moja ya vipindi vyake vya mafanikio, ambapo tumeshinda mataji manane,” Atletico ilisema.
Simeone mwenye umri wa miaka 53 ameisaidia Atletico kushinda ligi mbili za Uhispania, moja ya Copa del Rey, Europa League mbili, Super Cup mbili za Uropa na Super Cup moja ya Uhispania. Pia aliiongoza klabu hiyo kwenye fainali mbili za Ligi ya Mabingwa.
Kiungo huyo wa zamani ameifundisha Atletico katika michezo 642, akishinda 380 kati ya hiyo. Ndiye kocha mwenye michezo rasmi zaidi katika uongozi wa klabu, na ambaye amefundisha timu moja kwa misimu mingi mfululizo katika ligi ya Uhispania.
Tangu msimu wake wa kwanza kamili kwenye usukani, Atletico imefuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kila mara.
Maelezo ya kifedha ya mkataba mpya na hayakutolewa mara moja.