Mamlaka ya Palestina iko tayari kuchukua majukumu huko Gaza, rais wa Palestina amesema.
Mahmoud Abbas alisema mamlaka hiyo iko tayari kuchukua nafasi ya Hamas katika ukanda huo kama sehemu ya suluhisho la kina la kisiasa kwa Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki na Gaza.
Mnamo 2007, Hamas walichukua nafasi kutoka kwa Chama cha Fatah (kinachodhibiti Mamlaka ya Palestina) baada ya mapigano makali.
Hamas imekuwa serikali tangu wakati huo – ikiendesha utumishi wa umma na kutekeleza majukumu ya serikali kama vile afya na usafi wa mazingira – ingawa haijaruhusu uchaguzi mwingine.