Israeli imekubali wito wa kusitisha mashambulio yake kaskazini mwa Gaza ilikuruhusu baadhi ya raia kuondoka katika maeneo yanayoshudia mapigano mazito.
Rais wa Marekani Joe Biden aliwaambia waandishi wa habari kwamba aliiomba Israel “kusitishwa kwa zaidi ya siku tatu” wakati wa mazungumzo ya kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na kundi la Palestina Hamas, lakini akafutilia mbali uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano kwa jumla.
Kirby aliweka wazi kuwa hakutakuwa na usitishaji vita kati ya Israel na Hamas, akisema ungesaidia kundi la Palestina “kuhalalisha walichofanya” Oktoba 7, “na kwa kweli hatutasimamia hilo kwa wakati huu”.
Licha ya kutangaza hatua hiyo, waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema hatua yoyote ya kusitisha mapigano haimaanishi wamejisalimisha kwa Hamas.