Imeelezwa kuwa Hali ya upatikanaji wa Maji katika Mji wa Geita haijafikia 95% ya Malengo waliyojiwekea na Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) ambapo Uhakika wa huduma ya Maji kwa sass katika Mji wa Geita ni 75% .
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita , Frank Changawa wakati wakuiaga Bodi mpya ya Maji na kuikaribisha Bodi nyingine ambapo amesema ukamilishwaji wa Miradi utakapokamilika kufikia mwaka 2025 utasaidia kufikia Malengo waliyojiwekea ya kupata huduma ya maji kwa 95%.
“Kwa sasa Mamlaka yetu hali ya upatikanaji Maji hatujafikia Asilimia 95 kama malengo yanavyotutaka tuko asilimia 75 lakini tuna miradi ambayo inaendelea kuhakikisha tunafika lengo hilo 2025 , ” Mhandisi Chang”awa.
Cornel Magembe Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita katika Hafla hiyo ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) kwa hatua waliyofikia ya utoaji huduma ya maji katika Mji wa Geita kwa Asilimia 75 huku akiwqtaka kufikia Malengo ya waliojiwekea.
“Kazi hii ya kutosumbuliwa na kuambiwa shida kubwa ya maji na namna ya upatikanaji wa changamoto za maji leo nimejilidhisha kwamba ni kwasababu ya kazi nzuri ya Bodi ambayo lakini pamoja na Mkurugenzi na watumishi wengine ambao wanaemdelea kuidumia Bodi yetu , ” Mwakilishi wa RC. Geita.