Idadi ya wapalestina waliouawa kutokana na mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia 11,180 tangu mapigano yalipozuka Oktoba 7 mwaka huu.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika Kituo cha Matibabu cha Shifa, mkurugenzi wa ofisi ya habari ya serikali ya Gaza Bw. Ismail Al-Thawabteh amesema, kati ya watu waliouawa, kuna watoto 4,609 na wanawake 3,100, wengine zaidi ya elfu 28 wamejeruhiwa.
Ameongeza kuwa, kutokana na mashambulio ya Israel na ukosefu wa mafuta kwa mashine za kuzalisha umeme, hospitali 22 na vituo 49 vya afya katika Ukanda wa Gaza vimesitisha kutoa huduma.
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP liliripoti kuwa, ofisi zake zilizopo Gaza zimeshambuliwa katika shambulio la anga la Israel, na kusababisha vifo na majeruhi ya wakimbizi wa Palestina waliotafuta hifadhi katika ofisi hizo.