Zaidi ya watu 30 wamenasa baada ya mtaro wa barabara iliyokuwa chini ya ujenzi kuporomoka nchini India.
Mtaro huo uliporomoka siku ya Jumapili baada ya maporomoko ya ardhi katika jimbo la Uttarakhand kaskazini mwa India la Himalaya – eneo maarufu kwa watalii.
Wote walionaswa walikuwa wakifanya kazi kwenye handaki hilo, kulingana na maafisa, ambao walisema walikuwa wakisukuma oksijeni kupitia bomba kwenye sehemu iliyoanguka ili kusaidia wafanyikazi kupumua.
Chakula pia kinatumwa kwa wafanyikazi walionaswa.
Manohar Tamta, afisa wa usaidizi wa jimbo la Uttarakhand, alisema itachukua “muda kuwatoa”.
Walakini, wafanyikazi hao wametuma ishara zinazoonyesha kuwa wako salama, kulingana na shirika la habari la Press Trust la India, likimnukuu afisa wa serikali ya jimbo.