Baraza la ushindani nchini FCT limeridhia mchakato wa uunganishaji kampunu ya saruji ya tanga na ile ya twiga huku wanachama wa kampuni ya saruji ya tanga nao wakipitsha maamuzi ya kuruhusu uuzaji hisa asilimia 73 za kampuni hiyo kwenda kwa mwekezaji heidberg ambaye ndiye mmiliki kiwanda cha twiga cement.
Maamuzi hayo yamepitishwa leo jijini Dare slaamu na wana husa wa kampuni yabsaruji yabtanga ambapo akizungumza mwenyekitibwa bodi wa kampuni ya tanga cement patrick rutabanzibwa amesema maamuzi ya wana hisa hao yametokana na hali ngumu inayo ipitia kampuni ya tanga cemwnt ambalo imeshindwa kutoa gawio kutokana na deni ambalo lipo kwenye kampuninhuyo huku oia ikielemewa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo kujikuta wakihitaji zaidi uwekezaji kutoka kampuni ya heidelberg inayo miliki kampuni ya scancem ambaye ndie mmiliki wa kiwanda cha twiga cement.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya african mauritus ambaye anamiliki hisa zaidi ya asilimia 73 ya kiwand cha tanga cement reinhardt swart baye ndie mkurugenzi wa kiwanda cha tanga cement amesema mchakato wa upatikanaji wa mwekezajinhuo utakamilika haraka iwezekanavyo ili kuongeza nguvu yabuzalishaji ambapo pia ameiomba swrikali kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa uhai wa viwanda nchini
Hata hivyo tve imezungumza na baadhi ya wana hisa wa kiwanda cha tanga cement ambao wameeleza kusikitishwa na kukosa gawio kwa muda mrefu huku wakibariki kuuzwa kwa hisa hizo na kuunganishwa kwa kiwanda cha tanga cement na twiga cement ili kuwa kiwanda kimoja kitakacho kuwa imara .