Mashindano ya Bulaya Cup 2023, yanayodhaminiwa na Mbunge Esther Bulaya amefikia tamati mara baada ya kudumu kwa mwezi mmoja katika wilaya ya Bunda, huku wapenzi wa michezo mjini Bunda wakionesha kufurahishwa na kitendo hicho.
Bulaya Cup imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa vijana wa kike na wakiume sambamba na michezo mingine kama mchezo wa Bao, Draft, Pool table pamoja na mbio za Baiskeli kwa wenye ulemavu.
Katika kuhitimisha michuano hiyo iliyochezwa uwanja wa Sabasaba mjini Bunda, Mbunge Halima Mdee alikuwa mgeni rasmi pamoja na zawadi zingine kwa washindi ana ahidi kutoa laki moja kwa kila goli kwa wafungaji wa mpira wa miguu huku akihamasisha wapenzi wa michezo kuja mikoa ya Kanda ya ziwa kwani kuna vipaji vingi ila vinakosa mahali wanapoweza kuonesha uwezo wao ili kufikia ndoto zao.
Pamoja na zawadi zingine kwa washindi katika michezo mingine, mshindi wa kwanza wa mipira wa miguu kwa wanaume timu ya Bunda Kinds amezawadiwa kiasi cha fedha milioni mbili taslimu huku mishindi wa pili timu ya Sazila wamezawadiwa kiasi cha milioni moja.