Mataifa wa Morocco, Hispania na Ureno kupitia vyama vyao vya soka yamekutana leo Oktoba 28 2023 Rabat nchini Morocco na kusaini makubaliano ya kuomba uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2030.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Rais wa Chama cha soka Morocco Fouzi Lekjaa, Rais wa Chama cha soka Ureno, Fernando Gomes pamoja na Rais wa. Chama cha soka Hispania Pedro Rocha na wameshauriana namna watakavyofanya kwa pamoja kama wenyeji.
Miaka 100 ya michuano ya Kombe la Dunia Mataifa matatu yatataka kuweka historia ya kuunganisha utamaduni, maarifa pamoja na Ubunifu katika michuano hiyo.
Kama wazo hilo likifanikiwa basi michuano ya Kombe la Dunia itaandika histori ya kufanyika kwa mara ya kwanza katika Mabara mawili tofauti (Ulaya na Afrika).