Rapa wa Marekani Rick Ross amekuwa mtu mashuhuri hivi karibuni zaidi kununua ndege ya kibinafsi, akiipost mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii mapema mwezi huu Gulfstream G550.
Ndege hiyo imesajiliwa kama N676AS na inaendeshwa na injini mbili za Rolls-Royce.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, rapa Rick Ross hivi kupitia insta story yake ametumia kutangaza fursa ya kipekee ya kazi ya mhudumu wa ndege binafsi wa Maybach Air.
Kinachoshangaza wengi kwenye fursa hii ni mshahara wa kuvutia ambao Ross yuko tayari kutoa, unaofikia hadi $115,000 sawa na zaidi ya pesa za Kitanzania million 287.
Ross,hufanya safari za mara kwa mara kwa sababu ya ratiba yake ngumu na ubia mkubwa wa biashara, alionyesha hitaji lake la mhudumu wa ndege mwenye uzoefu.
Kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii, alishiriki maelezo ya nafasi hiyo.
. “Yo wassup ”
“Nyuma yangu kuna Maybach air G550, na kwa mara ya kwanza kabisa, Ricky Rozay anatafuta mhudumu wake mwenyewe wa ndege. Mhudumu wangu binafsi ndani ya ndege mshahara wake utakuwa mzuri hadi $115,000.”
‘Unatakiwa uwe na uzoefu na mchangamfu na mwenye kuwa na uhitaji na namna ya kuhudumia kwenye ndege nitaacha email yangu nasisistiza nahitaji mtu serious na mchangamfu’..