Wataalamu wa mifumo ya kijiografia (GIS), Taasisi za Serikali, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa teknolojia wanatarajia kuktana leo tarehe 15 jijini Dar es salaam katika kumbi za Tume za sayansi na teknolojia (COSTECH) kwa jailli ya mafunzo na kueleza namna GIS inavyotumika katika matumizi ya kiramani na kijiografia kwa sekta mbalimbali ambazo zimeingia kwenye mfumo huo katika kupunguza changamoto za upatikanaji wa masuala mbalimbali.
Maadhimisho hayo yatakuwa ya siku mbili kuanzia Novemba 15, 2023 na yanatarajiwa kuhudhuriwa na watu 250 kutoka sekta mbalimbali ambapo siku ya kwanza kutakuwa na majadiliano pamoja na maonyesho na siku inayofuata kutakuwa na mafunzo ya utumiaji wa Gis kwa wasiofahamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la RootGis, Antidius Kawamala amesema maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na maonyesho ya sekta ya kilimo,madini na Uvuvi ili kuonyesha urahisi wa upatikanaji wa masuala yanayohusu sekta hizo.
“Maonyesho hayo yatatoa fursa kwa watu kujifunza namna ya utumiaji wa mifumo katika upatikanaji wa ardhi yenye rutuba na ufikiwaji wa mashamba kwa ajili ya kilimo, maeneo yenye madini kwa wachimbaji wadogo, upatikanaji wa mabomba ya maji safi na mazalia ya samaki kwa wavuvi wa baharini na ziwani,”amesema Kawamala. Amesema hayo yote yataelezwa na wataalamu kutoka katika sekta husika pia kutakuwa na wadau kutoka sekta binafsi na mtu moja moja watakaofundisha kuhusiana na GIS.
Kwa upande wake muwakilishi wa shirika la Youthmappers Tanzania,Erick Mnyali amesema maadhimisho hayo yanakwenda kusogeza wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kujifunza namna ya teknolojia ya kijiografia inaweza kuwasaidia katika shughuli mbalimbali.
“Uwepo wetu katika maadhimisho haya yatawasaidia wanafunzi wa vyuo ambao hawajajiunga katika programu zetu maana Tanzania tuna vyuo 22 vilivyojiunga huku Dar es Salaam tukiwa na vyuo saba,”amesema Mnyali. Naye, kiongozi wa Ufundi wa Buni Innoviation Hub iliyopo chini ya Costech, Patricia Pastory amewaomba vijana wanao vutiwa na masuala ya Sayansi na teknolojia wawepo ili kujifunza masuala yatakayowasaidia kwenye ubunifu.” -Erick Mnyali muwakilishi wa shirika la Youthmappers