Wakati United wamemuunga mkono Ten Hag kuhusu mzozo wake na Sancho, klabu hiyo inatambua kwamba imepunguza kwa kiasi kikubwa thamani ya soko ya winga huyo.
Saudi Arabia imetajwa kuwa ni uwezekano mwingine Januari na msimu ujao wa joto,kumtaka Sancho ingawa yeye angependelea kusalia Ulaya katika hatua hii ya kazi yake ikiwezekana.
Al-Ettifaq ilijiondoa kwenye mkataba wa mkopo mwishoni mwa dirisha la majira ya kiangazi kwa sababu klabu inayonolewa na Steven Gerrard haikujitolea kumnunua kwa kudumu kwa pauni milioni 50 mwishoni mwa msimu.
Wanne wakubwa wa Saudia wa Al-Nassr, Al-Ittihad, Al-Ahli na Al-Hilal wanaweza kuwa sokoni kwaajili ya Sancho, wakati Ettifaq na Al-Shabab wanaweza kuibuka kama chaguo katika msimu wa joto.
Njia mbadala ya Sancho ni kusubiri na kuona kama hali yake itabadilika akiwa United mara Sir Jim Ratcliffe na Ineos watakaponunua klabu hiyo – mchakato wa pauni bilioni 1.4 ambao unapaswa kukamilishwa kabla ya mapumziko ya kimataifa kumalizika.
Wawakilishi kutoka Juventus walikuwa nchini Uingereza wiki iliyopita na inafahamika kuwa walifanya mawasiliano na United kuhusu uwezekano wa kumnunua Sancho kwa mkopo mwezi Januari pia.
Haiwezekani Waitaliano hao wangeweza kumudu ada ya uhamisho kwa mchezaji ambaye aliigharimu United pauni milioni 73 kutoka Borussia Dortmund mnamo 2021 na alipatikana kwa pauni milioni 45 msimu wa joto.