Shirika la Afya Ulimwenguni limepoteza mawasiliano na wafanyikazi wake wa afya katika hospitali ya al-Shifa katika Ukanda wa Gaza, ambayo imevamiwa na jeshi la Israeli, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kwenye mtandao wa kijamii.
“Ripoti za uvamizi wa kijeshi katika hospitali ya Al-Shifa zinatia wasiwasi sana. Tumepoteza mawasiliano tena na wahudumu wa afya hospitalini. Tuna wasiwasi mkubwa kwa usalama wao na wa wagonjwa wao, “alisema.
Wanajeshi wa Israel waliingia katika hospitali ya al-Shifa katika kile inachosema ni operesheni iliyolengwa dhidi ya maeneo yanayodaiwa kuwa ya Hamas chini ya jengo hilo.