Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amewataka Watanzania kuendelea kuwaeshimu na kuwathamini Familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwani Wazazi wao waliacha kutumia muda mwingi kwaajili yao na wakautumia kwaajili ya kulipambania Taifa letu la Tanzania.
“Naomba nitoe rai kwa Watanzania hizi familia kuna mambo waliyakosa kwasababu ya ushiriki wao katika kujitoa kwa Watanzania kwahiyo tunapokutana nao na kuwaona tuwaheshimu kwani Wazazi wao hawakuwatumikia wao bali waliwatumikia Watanzania kwahivyo lazima waheshimike” Alisema Mwenezi Makonda.
Pia, Mwenezi Makonda ametoa shukrani kwa Familia kwa mapokezi mazuri.
“Namshukuru sana Mungu kwa kupata Afya njema na kufika hapa, naishukuru Familia kwa mapokezi mazuri na kupata fursa ya kulala hapa na hata usingizi ulikuwa mzuri na niliota ndoto njema” Mwenezi Makonda.
“Si tu kama utamaduni wa kila Kiongozi kufika hapa ila nimekuja kuwaambia kuwa tupo oamoja katika kuenzi na kueshimh kazinya Hayati na Maneno haya ninamaanisha kwamba Mwalimh nitamuezni kwelikweli” Alisema Mwenezi Makonda.