Ethiopia siku ya Jumatano “ilikaribisha” tangazo kwamba Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) litarejelea utoaji wa msaada wa chakula kote nchini, uliositishwa mwezi Juni, kufuatia kuhitimishwa kwa makubaliano ya kufuatilia usambazaji wa misaada.
USAID ilitangaza Jumanne kwamba itaanza tena utoaji kutoka mwezi ujao, kwa kipindi cha awali cha mwaka mmoja, ambapo shirika hilo litafuatilia kama taifa la Ethiopia linatimiza ahadi zake, dhidi ya hali ya nyuma ya shutuma kwamba msaada umeelekezwa kuwanufaisha wanajeshi.
“Tunakaribisha uamuzi wa USAID wa kurejesha msaada wa chakula kwa Ethiopia. Ni muhimu kuharakisha mchakato wa kurejesha msaada wa chakula ili kuwafikia wale wote wanaohitaji,” alisema Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Demeke Mekonnen kwenye X (ex-Twitter) .
Mwezi Juni, Addis Ababa ilikosoa kusitishwa kwa msaada wa chakula na wakala wa Marekani, uamuzi ambao pia ulichukuliwa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kwa sababu ya ubadhirifu, kwa madai kwamba “unaadhibu mamilioni ya watu”.
USAID ilikuwa tayari imetangaza mwanzoni mwa Oktoba urejeshaji mdogo wa utoaji wa msaada wa chakula ili kukidhi mahitaji ya maelfu ya wakimbizi katika nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.
Kurejeshwa huko kulihusu baadhi ya kambi thelathini nchini Ethiopia, ambayo inahifadhi karibu wakimbizi milioni moja, hasa kutoka Sudan Kusini, Somalia na Eritrea.
Takriban watu milioni 20, sawa na asilimia 16 ya wakazi milioni 120 wa Ethiopia, wanategemea msaada wa chakula, kama ilivyokadiriwa na shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu (Ocha) mwishoni mwa Oktoba, kutokana na migogoro na ukame wa kihistoria katika eneo la Pembe ya Afrika. wamewakimbia watu milioni 4.6 kote nchini.