Msanii na mwanamuziki Alexandra Skochilenko amepatikana na hatia ya kusambaza habari za uwongo akijua kuhusu tabia ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Mnamo Machi 2022, kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 alibadilisha vitambulisho vya bei katika duka kubwa huko St Petersburg na vipande vidogo vya karatasi akitaka vita vya Urusi vikomeshwe nchini Ukraine na kukosoa mamlaka.
Mahakama ya Urusi sasa imemhukumu kifungo cha miaka saba katika gereza moja.
Alikanusha shtaka rasmi la kueneza habari za uwongo kwa makusudi kuhusu jeshi.