Operesheni inayoendelea ya Israel katika hospitali kubwa zaidi ya Gaza, Al-Shifa, inajiri huku wizara ya afya ya Palestina yenye makao yake makuu mjini Ramallah ikionya kuwa hospitali 26 kati ya 35 za Gaza hazifanyi kazi tena. Inasema tisa zilizobaki “zinafanya kazi kwa sehemu”.
Hili sio onyo la kwanza la aina yake. Hapo jana maafisa wa Hamas huko Gaza walisema hospitali 25 hazitumiki. Na Ijumaa iliyopita, Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema kwamba theluthi mbili ya hospitali katika Ukanda wa Gaza “hazifanyi kazi hata kidogo”.
Wizara ya afya ya Palestina ni sehemu ya Mamlaka ya Palestina, yenye makao yake katika Ukingo wa Magharibi – na haina udhibiti wowote juu ya Gaza.