Kando na kuwa mmoja wa wachezaji bora wa kufunga uwanjani, mchezaji wa Manchester City Kevin De Bruyne anaonyesha kuwa anaweza kusaidia pia katika utunzi wa ngoma kali.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 amepewa sifa za kuandika kwenye project mpya ya Drake ‘Scary Hours 3’ kwa mchango wake kwenye mojawapo ya nyimbo hizo.
Chini ya miezi miwili baada ya kuachia albamu yake ya nane ya studio, ‘For All the Dogs’, rapa kutoka Canada Drake alitoa EP yenye nyimbo sita kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wake.
‘Scary Hours 3’, kama jina linamaanisha, ni toleo la tatu la Rap-Heavy Extended Plays, na kwa toleo hili, Drake alimuajiri mchezaji wa Manchester City Kevin de Bruyne na kulingana na Spotify, wimbo wa nne kwenye project ya ‘Wickman’ una mkono wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea kama mmoja wa waandishi.
Kwa sasa De Bruyne yuko nje ya dimba katika klabu ya Manchester City huku akiuguza jeraha la sehemu ya misuli
Anatarajiwa kurejea baadaye mwakani, na kulingana na Pep Guardiola, “anajisikia vizuri,” lakini Mhispania huyo anasema klabu haitamharakisha.