Baraza la mawaziri la vita la Israel limeidhinisha kuruhusu lori mbili za mafuta kwa siku kuingia Gaza ili kusaidia mahitaji ya Umoja wa Mataifa, afisa wa Israel amesema.
Afisa huyo, ambaye alikataa kutambuliwa, alisema mafuta yatatoa msaada “mdogo” kwa maji, maji taka na mifumo ya usafi huko Gaza ili kuzuia milipuko, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Uamuzi huo ulikuja baada ya ombi kutoka Washington, afisa huyo alisema.
Shirika la Afya Ulimwenguni limesema “lina wasiwasi mkubwa” juu ya kuenea kwa magonjwa huko Gaza, huku kuwasili kwa msimu wa baridi kukiwa na hali mbaya zaidi. (Angalia chapisho la 10.55).
Wakati huo huo, Human Rights Watch imesema ukosefu wa maji safi unamaanisha magonjwa ya kuambukiza yanayosambazwa na maji kama vile kipindupindu na typhoid yataanza kuenea hivi karibuni.