Mapigano kati ya wapiganaji mamluki wa jeshi la Ukraine kwenye tafrija iliyofanyika katika mji wa Kiev yamejeruhi raia kadhaa wa Marekani, Canada na Romania.
Tukio hilo lilijiri baada ya mamluki kadhaa kutoka kitengo cha askari wa kigeni cha jeshi la Ukraine kupigana wao kwa wao kwenye tafrija iliyofanyika kusini mashariki mwa Kyiv.
Ripoti zinasema, raia mmoja wa Uingereza pia aliwashambulia wenzake kwa kisu na kuwajeruhi kadhaa katika mapigano kati ya askari hao mamluki waliokuwa likizoni.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa, yanaonyesha kuwa asilimia 50 ya vikosi vya jeshi la Ukraine ni mamluki wa kigeni.
Awali shirika la habari la Sputnik liliripoti kuwa, maelfu ya mamluki kutoka nje wanahudumu ndani ya jeshi la Ukraine na kwamba asilimia 50 ya mamluki hao wanahudumu katika jeshi la nchi hiyo.
Shirika la habari la Sputnik aidha limeripoti kuwa, wanajeshi zaidi ya elfu 90 wa Ukraine wameuawa katika vita vya nchi hiyo na moja ya sababu za kuendelea vita nchini humo ni kuwepo maelfu ya mamluki wa nchi ajinabi katika jeshi la Ukraine.