Wataalamu kutoka Taasisi ya Weill Cornel ya nchini Marekani wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa lengo la kujionea miundombinu ya kutolea huduma na kukutana na wataalamu ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa taasisi hiyo kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila) kuimarisha kitengo cha kutibu kiharusi (Stroke Unit)
Awali wataalamu hao walikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ambaye
alisema kuwa mpango huo utakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia matibabu kwa watu waliopata kiharusi ndani ya saa 24 za mwanzo.
Alisema kuwa Muhimbili inavifaa tiba vya kisasa vya kuhudumia wagonjwa wa kiharusi ikiwemo mtambo wa Angio-Suite ambao hutumika kufanya uchunguzi na matibabu ya kiharusi, pamoja na wataalamu wabobezi wa kutibu kiharusi.