Mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Israel amesema katika taarifa yake kuwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza hawataachiliwa huru hadi Ijumaa.
Hakuna mateka wa Israel anayeshikiliwa na Hamas atakayeachiliwa kabla ya Ijumaa, alitangaza mkuu wa Baraza la Usalama la Taifa la Israel, Tzachi Hanegbi, wakati makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa kundi la kwanza la mateka viikuwa vikikitarajiwa leo Alhamisi.
“Mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wetu yanaendelea bila shaka.” Zoezi hili la kuachiliwa kwa mateka litaanza “siku ya Ijumaa”, amesema usiku katika taarifa, bila kutoa maelezo.
Hakutakuwa na maelewano katika mapigano kati ya Israel na kundi la wapiganaji la Hamas kutoka Palestina kabla ya Ijumaa, kinyume na wahusika wakuu walivyotangaza awali, afisa wa Israel pia ameliambia shirika la habari la AFP.