Mafuriko makubwa yamekumba miji na jamii nchini Somalia, na kusababisha uharibifu mkubwa na kuwaacha watu milioni 1.7 wakihitaji msaada, kulingana na mashirika ya misaada ya kibinadamu.
Mji wa kati wa Somalia wa Beledweyne, ambao uko katika eneo linalovuka Mto Shabelle, umeathiriwa pakubwa na mafuriko ambayo yamekumba maeneo kadhaa ya nchi.
Miongoni mwa mamia na maelfu ambao wamekuwa wakiteseka ni Hakima Mohamud Hareed, mama wa watoto wanne.
Familia yake ilikuwa hivi majuzi ilikimbia mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab kutafuta usalama na utulivu.
Hakima na familia yake waliishi Kutiimo, kambi ya IDPs huko Beledweyne, lakini hali ya hewa kali iliharibu hema lake dogo ambalo lilikuwa na ulinzi mdogo.
Mvua ilinyesha kwa kasi kutoka pande zote, ikipita kwenye kitambaa chembamba na kudhoofisha mali waliyokuwa nayo na nyumba ya muda waliyojihifadhi.
“Nyumba zetu zilizingirwa na mafuriko tulipokuwa tukipanga, na mali zetu zote zilisombwa na mafuriko, hivyo tulitoroka tu na maisha,” alisema.
Maji ya mafuriko yaliposonga katika jiji hilo, nyumba zilisombwa na maji, na watu walilazimika kutafuta hifadhi kwenye maeneo ya juu.
Kulingana na Shashwat Saraf, Mkurugenzi wa Dharura wa Afrika Mashariki katika Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC), hekta milioni 1.5 za ardhi nchini Somalia zilikumbwa na mvua hiyo.