Zaidi ya Billioni 55 zimetolewa na serikali kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji wilayani Iringa ili kuongeza Tija ya uzalishaji wa mazao .
Katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa , Joseph Lyata Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama cha mapinduzi na amesema kumekuwa na ushindani wa masoko hapa nchini hivyo wameweka skimu hiyo kwa wakulima ili waweze kuwekeza.
“ skimu hii itaongeza ajira kwa vijana na wakulima na itasaidia pia wakulima kupata kipato kikubwa kitakacho watoa kwenda kwenye hatua ndogo kwenda kuwa wakulima wakubwa na hatahivyo serikali yetu hii ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu imetoa fedha katika kutekeleza maendeleo hususan sekta ya kilimo , Elimu , maji Miundombinu ya barabara pamoja hata na Afya “ alisema Lyata
Hatahivyo Lyata Ameendelea kusema upatikanaji wa maendeleo unategemea miundombinu imara na amesisitiza kuwa kuna ulazima wa kuwa na miundombinu imara ambayo itachangia ukuaji wa sekta ya kiuchumi katika kilimo na biashara .
“ sisi kama chama tumekuwa tukitekeleza ilani yetu na kuhakikisha tunaimarisha miundombinu ili kuwafanya wakulima walio vijijini kuweza kusafirisha biashara zao au mazao yao kwenda maeneo mbalimbali “
Aidha Lyata amewaagiza viongozi kuanzia ngazi ya mtaa adi wa Chama kufanya mikutano ya hadhara ili kuelezea maendeleo yanayotekelezwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi .